Tunda Ajianika na Njemba Mpya Baada Ya Tetesi Kutemana na Casto - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Tunda Ajianika na Njemba Mpya Baada Ya Tetesi Kutemana na Casto

Video vixen maarufu Bongo Tunda Sebastian ameingia Kwenye headlines baada ya kupotea picha ya mwanaume Kwenye mitandao ya kijamii baada ya Tetesi za kuachana na Mtangazaji wa Clouds Tv, Casto Dickson.


Tunda na Casto walikuwa Kwenye Mahusiano kwa Miezi michache sasa lakini wiki iliyopita kuna taarifa zilisambaa Kwenye mitandao ya kijamii kuwa wawili hao hawapo Tena.


Global Publishers waliripoti kuwa Tunda kamtosa kabisa Casto taarifa ambazo Casto alizikataa na kudai wapo wote bado lakini alipotafutwa Tunda aliweka wazi kuwa yupo single.


Tunda ameendelea kuchochea tetesi hizo baada ya kuposti screenshot ya FaceTime call yake na mwanaume mwingine ambaye hajatambulika bado mpaka hivi sasa.


Kupitia ukurasa wake wa Snapchat Tunda aliweka picha hii ambayo inasambaa Kwenye mitandao ya kijamii na kuwafikirisha watu kuwa huenda Tunda amemtosa Casto na kuweka kambi kwa jamaa huyu: 


The post Tunda Ajianika na Njemba Mpya Baada Ya Tetesi Kutemana na Casto appeared first on Ghafla!Tanzania.... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More