TUNDU LISSU AFUNGUKA KUHUSU MSHAHARA NA KURUDI TANZANIA - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TUNDU LISSU AFUNGUKA KUHUSU MSHAHARA NA KURUDI TANZANIA

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amedai kuwa uongozi wa Bunge la Tanzania umemlipa madai ya mishahara yake aliyokuwa akidai ya Januari hadi Machi 2019.
Amesema hayo leo Alhamisi Aprili 18,2019 kupitia ujumbe mfupi aliouweka katika mitandao ya kijamii akizungumzia afya yake na madai yake ya mishahara.

Lissu aliyeko Ubelgiji kwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 Septemba 7, 2017 mbali na mshahara wake pia amezungumzia afya yake akisema,“Na kwenye hili habari ni njema sana. Tarehe 2 ya mwezi huu nilikutana na madaktari wangu kwa appointment ya kwanza tangu operesheni za tarehe 20 Februari.”

“Taarifa yao ni kwamba mfupa wote wa mguu wa kulia umepona vizuri. Sehemu iliyowekewa 'kiraka' cha mfupa na kupigwa 'ribiti' ya chuma juu kidogo ya goti; na sehemu ya kwenye paja iliyotakiwa kuota mfupa mpya, zote ziko vizuri.”

“Sasa kazi kubwa iliyobaki ni kukunja goti na kujifunza kutembea tena. Naomba mniamini nikisema kujifunza kutembea tena, baada ya zaidi ... Continue reading ->

Source: Mwanaharakati MzalendoRead More