“Tusiishi Kwa Chuki na Uadui Maana Hatujui Kesho Yetu Itakuwaje”- Ommy Dimpoz - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

“Tusiishi Kwa Chuki na Uadui Maana Hatujui Kesho Yetu Itakuwaje”- Ommy Dimpoz

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Omary Nyembo Maarufu kama Ommy Dimpoz amefunguka na kuongelea hali yake ya kiafya baada ya kuumwa kwa zaidi ya Miezi mitano.


Jana ilikuwa ni siku ya kuzaliwa ya Ommy Dimpoz ambaye alikuwa hoi mahututi kwa Miezi michache iliyopita baada ya kufanyiwa upasuaji wa koo nchini South Africa.


Akiwa anasheherekea siku yake ya kuzaliwa Ommy Dimpoz ameweka ujumbe mzito ambapo pia ameweka picha yake alipokuwa hoi taabani ICU.


Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ommy Dimpoz ameandika umuhimu wa kutokuwa na vinyongo wala chuki na watu maana hakuna anayejua sana wala siku ya kufa.


View this post on InstagramLeo 13th September ni kumbukumbu yangu ya siku ya kuzaliwa. Namshukuru sana Mwenyezi Mungu (ALHAMDULILAAH) kwa kunipa nafasi ya kuuona mwaka mwingine, kwani niliyoyapitia katika kipindi cha takribani miezi 5 kama ingekuwa sio mapenzi yake yeye (M/Mungu) basi ingekuwa imebaki history. Nilichojifunza kipindi hichi chote ni kuwa kuumwa ni Ibada na sisi kama binadamu hatujakamilika leo unaweza kuwa mzima na kesho ukawa mahututi kitandani, ndio maana nimeamua kushare picha ambayo nilipigwa nikiwa ICU japo nafahamu sio kitu kizuri kupost picha kama hii kwenye mitandao ila nia yangu ni kujaribu kukumbushana sisi kama Binadamu kuwa kuna leo na kesho kwahiyo tusiishi kwa chuki na Uadui maana hatujui kesho yetu itakuwaje!! Kuna kipindi wakati nimelazwa nilikata tamaa ya kuishi nikaona labda muda wangu umekwisha lakini hapo Hospital akaletwa mgonjwa mwingine ambae alikuwa pembeni yangu alishambuliwa na majambazi kwa risasi tisa mwilini lakini madaktari wakafanikiwa kuokoa maisha yake na akapona so nikajiuliza mimi ni nani nikate tamaa ya kuishi na nikajifunza kwamba kuugua sio kufa, Ni vyema tukipata nafasi basi tuwaombee na kuwafariji wagonjwa kwani wanayoyapitia ni magumu mno. Kwasasa namshukuru Mwenyezi Mungu naendelea vizuri na bado niko kwenye recovering, pia nawashukuru watu wote ambao mmekuwa mkiniombea dua nipone kwa haraka kuanzia mashabiki mpaka wasanii wenzangu na kila mtu aliyeniombea kwa imani yake Nashukuru sana. Mungu awabariki sana. : Pia Shukran za dhati kwa Familia yangu, Marafiki zangu wa Karibu, Management yangu ROCKSTAR FAMILY @officialalikiba na my lovely Manager @sevenmosha ambaye amehangaika na mimi mfano wa Mama Mzazi na mtoto wake pamoja na my Big Brother Governor @joho_001 ambaye ameniuguza kwa kipindi hichi chote chini ya uangalizi wake na Madaktari kuanzia Kenya Mpaka South Africa. ASANTENI SANA NA INSHAALLAAH KWA UWEZO WA ALLAAH I WILL COME BACK STRONGER 💪🏽🙏❤


A post shared by Ommy Dimpoz (@ommydimpoz) on Sep 12, 2018 at 2:03pm PDT

The post “Tusiishi Kwa Chuki na Uadui Maana Hatujui Kesho Yetu Itakuwaje”- Ommy Dimpoz appeared first on Ghafla!Tanzania.


Source: Ghafla TZRead More