TUSIMAMIE WAKANDARASI WANAOJENGA MJI WA SERIKALI DODOMA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TUSIMAMIE WAKANDARASI WANAOJENGA MJI WA SERIKALI DODOMA

Manaibu Mawaziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wamefanya ziara ya kutembelea na kukagua kiwanja kilichotolewa kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Wizara hiyo ambapo Serikali imetoa shilingi bilioni moja kwa kila Wizara na kuelekeza kuwa ifikapo mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka huu Wizara zote ziwe zina majengo yake ya ofisi kwenye mji wa Serikali uliopo Ihumwa mkoani Dodoma.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa akiambatana na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akiwa na Katibu Mkuu wa Mawasiliano Mhandisi Dkt. Maria Sasabo na wataalamu wa Wizara hiyo wametembelea na kukagua eneo lenye ukubwa wa ekari 6.3 ambalo limetengwa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano lililopo Ihumwa mkoani Dodoma ambalo litagharimu jumla ya shilingi bilioni 1.120 na litajengwa na Vikosi vya Ujenzi, tawi la Dar es Salaam.

Kwandikwa amesema kuwa Serikali imetupa dhamana kubwa ya kuwa wakandarasi na kusimamia majengo ya Wizara zote, ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More