UBALOZI WA CHINA NCHINI WAINUA VIJANA KUPITIA WUSHU - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

UBALOZI WA CHINA NCHINI WAINUA VIJANA KUPITIA WUSHU

*Vijana wapata fursa ya kujifunza na kujiajiri wenyewe, waushukuru ubalozi wa China nchini

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
BARAZA la michezo nchini (BMT) kwa kushirikiana na chama cha Wushu pamoja na vituo vya lugha ya kichina katika vyuo vikuu vya Dodoma na Dar es Salaam wameendesha mashindano ya kimataifa ya sita ya Wushu jijini Dar es Salaam kwa kuwakutanisha washiriki 200 kutoka nchini Tanzania na washiriki 20 kutoka nchini Rwanda.

Akizungumza mara baada ya mashindano hayo  mgeni rasmi wa shughuli hiyo ambaye ni mwakilishi wa katibu mkuu wa baraza la michezo la taifa (BMT) Milinde Mahona amesema kuwa ubalozi wa China nchini umekuwa ukifanya jitihada za ziada katika michezo na chama cha Wushu kipo kwenye orodha ya vyama vinavyofanya vizuri na hiyo ni kutokana na uongozi bora na ameupongeza ubalozi wa China nchini kwa ushirikiano wanaoonesha kwa vijana hao.

Amesema kuwa ubalozi wa China nchini umekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha na kushirikiana na  vijana katika suala la kujiajir... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More