UBALOZI WA CHINA WAMKABIDHI ZAWADI DK.TULIA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

UBALOZI WA CHINA WAMKABIDHI ZAWADI DK.TULIA


*Ni kwa ajili ya washindi wa Tulia Traditional Dances Festival Na Said Mwishehe,Globu ya jamiiMKURUGENZI wa Taasisi ya Tulia Trust Dk.Tulia Akson ameushukuru Ubalozi wa China nchini Tanzania kwa kumkabidhi pikipiki 10 kwa ajili ya washindi watakaopatikana kwenye tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2018.
Dk.Tulia ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge amekabidhiwa pikipiki hizo leo katika ubalozi huo na Mwakilishi wa Balozi wa China Tanzania nchini Xu Chen.Thamani ya pikipiki hizo ni Sh.milioni 21,600,000.
Akizungumza baada ya kupokea pikipiki hizo Dk.Tulia amesema anaushukuru ubalozi huo kwa kutoa zawadi hizo kwa ajili ya washindi wa tamasha hilo litakalofanyika kuanzia Septemba 18 hadi Septemba 22 mkoani Mbeya.
“Kwa niaba ya Taasisi ya Tulia Trust tunatoa shukrani zetu kwa ubalozi wa China nchini Tanzania kwa namna ambavyo wamekuwa pamoja nasi kwa kutoa zawadi kwa ajili ya washindi.
“Mwaka jana walitoa pikipiki 10 ambazo tulikabidhi kwa washindi.Lengo la tamasha hili ni kukuza ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More