Uchaguzi wa Marekani katikati ya muhula unamaanisha nini ? - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Uchaguzi wa Marekani katikati ya muhula unamaanisha nini ?

Wamarekani wameanza kupiga kura katika uchaguzi wa kitaifa wa katikati ya muhula ambao unaonekana kama kura ya maoni kuhusu urais wa Donald Trump.


Vituo vya kupiga kura vimefunguliwa kwenye Pwani ya Mashariki huku vyama vya Republican na Demoratic vikipania kuchukua udhibiti wa mabunge ya uwakilishi na Seneti. Uchaguzi huu wa katikati ya muhula unakuja wakati rais Trump amefikia nusu ya muda wa uongozi wake madarakani.Uchaguzi huo pia unatarajiwa kubaini ikiwa Trump ana uwezo wa kuongoza Marekani katika kipindi cha miaka miwili ijayo.Shauku ya upigaji kura inatarajiwa kuchochea watu wengi zaidi kushiriki zoezo hilo. Viti 435 katika bunge la waakilishi na viti 35 kati ya 100 katika Seneti vinakabiliwa na ushindani mkubwa.


Siku za hivi karibuni rais Trump amekuwa akitumia mbinu tofauti kuwasilisha hoja ambazo zinaonekana kuzua hisia mseto katika juhudi ya kuimarisha uungwaji mkono wake. Aliyekuwa mtangulizi wake, Barack Obama – amekuwa mstari wa mbele kuendesha kampeini za chama cha... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More