Uchebe Atangaza Vita Kwa Wanaume Wanaommendea Shilole - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Uchebe Atangaza Vita Kwa Wanaume Wanaommendea Shilole

Mume wa staa wa Bongo fleva na mjasiriamali Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole, Asharaf Uchebe amewachimba mkwara wanaume wowote ambao wanataka kuingilia ndoa yake na Shilole.


Uchebe amefunguka na kudai kuwa atakuwa tayari kwenda hata jela endapo atagundua kuwa kuna mwanaume anamtaka mke wake au hata atagundua kuwa anasalitiwa.Kwenye mahojiano na Ijumaa Wikienda , Uchebe alisema kuwa anajua anapata tabu gani kuhakikisha anailinda ndoa yake hivyo ataumia sana atakapomkuta mwanaume mwingine anamrubuni mkewe na anaweza kufanya kitu ambacho hakikutarajiwa na watu wengi.Mimi nampenda sana mke wangu najua wazi ni kiasi gani naumia kuilinda ndoa yangu isiingiliwe na kidudu mtu ila watu hawezi kuelewa hata kidogo hivyo kama nitamkuta mwanaume yeyote au nikimfumania mke wangu huyo mwanaume ama zake ama zangu”.Shilole na Uchebe walifunga ndoa mwaka jana mwishoni.


 


The post Uchebe Atangaza Vita Kwa Wanaume Wanaommendea Shilole appeared first on Ghafla!Tanzania.... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More