UDHIBITI MAPATO, NIDHAMU KWA WATUMISHI VIMEPAISHA UCHUMI-MAJALIWA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

UDHIBITI MAPATO, NIDHAMU KWA WATUMISHI VIMEPAISHA UCHUMI-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hatua ya kudhibiti upotevu wa mapato na matumizi ya fedha za Serikali, uboreshwaji wa mazingira ya biashara na uwekezaji pamoja na kusimamia uwajibikaji kwa watumishi wa umma kumesababisha kukua kwa uchumi.
Amesema Tanzania ni nchi yenye amani na utulivu na Serikali imeendelea kuongeza nguvu katika kudumisha amani na utulivu kwenye maeneo yote nchini, hali inayotoa fursa kwa wananchi wake kuendeleza shughuli zao za maendeleo. 
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatatu, Julai 8, 2019) wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Misri, Dkt. Mostafa Madbouly akiwa katika siku yake ya kwanza ya ziara yake ya kikazi nchini Misri.
Hivyo, amemuhakikishia Waziri Mkuu wa Misri kwamba Serikali ya Tanzanzia na wananchi wake wapo tayari kuendelea kushirikiana na Serikali ya nchi hiyo na wananchi wake katika kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi hizo mbili.
Amesema nchi za Tanzania na Misri zinahitaji kutumia nafasi ya ushirikiano wa kibiashara na uwekeza... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More