UFARANSA NA UJERUMANI ZAKUMBWA NA JOTO KALI - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

UFARANSA NA UJERUMANI ZAKUMBWA NA JOTO KALI


Nchi za Ulaya kaskazini zimekumbwa na joto kali lisilokuwa na kifani mnamo wiki hii. Mamlaka husika nchini Ujerumani na Ufaransa zimejiweka katika hali ya tahadhari.
Watalaamu wa mambo ya hali ya hewa wamesema, kuongozeka kwa viwango vya joto duniani ni ushahidi mwingine wa kuendelea kwa mabadiliko ya tabia nchi. Idara kuu ya hali ya hewa imesema kiwango cha joto leo kinatarajiwa kufikia nyuzi joto 38 hapa nchini Ujerumani.
Mtaalamu wa mambo ya hali ya hewa Sabine Krueger amesema viwango vya joto vinaweza kuvunja rekodi hadi kufikia nyuzi joto 40 kwenye baadhi ya maeneo ya Ujerumani kama vile sehemu zinazouzunguzka mji maarufu wa Frankfurt ulioko kwenye jimbo la kati la Hesse.Mnamo mwaka 2015 sehemu za jimbo la kaskazini, Bavaria zilifikia nyuzi joto 40.3. 
Hata hivyo mtaalamu huyo wa hali ya hewa Sabine Krueger amesema baadhi ya maeneo yatafikia nyuzi joto 29 tu hasa kwenye ukanda wa bahari ya kaskazini. Madaktari wana wasiwasi juu ya viwango hivyo vya joto.
Watu wakijipumzisha kwenye ma... Continue reading ->


Source: Mwanaharakati MzalendoRead More