UFARANSA YAAHIDI KUZIDISHA USHIRIKIANO NA TANZANIA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

UFARANSA YAAHIDI KUZIDISHA USHIRIKIANO NA TANZANIA

Na Khadija Khamis – Maelezo 
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavieter amesema nchi yake itaendelea kuongeza ushirikiana wake na Tanzania katika masula ya Uchumi, Kijamii na Utamaduni. Balozi Frederic Clavieter alieleza hayo katika Ofisi ya Jumuiya ya Ufaransa na Zanzibar Migombani alipofanya ziara ya kutembelea ofisi hiyo akiambatana na Maseneta watatu kutoka Ufaransa.

Maseneta waaliofutana na Balozi Clavieter ni Ronan Dantec kutoka Jimbo la Loire-Atlantique, Cyril Pellevat wa Jimbo la Haute-Savoie na Seneta Bernard kutoka Jimbo la Paris .Alisema katika kuimarisha ushirikiano huo, Ufaransa imeamua kuongeza msaada wake kwa Tanzania kutoka Euro milioni 50 kwa mwaka kufikia Euro milioni 100 ili kuharakisha maendeleo yake.

Alisema mahusiano kati ya Ufaransa na Tanzania ulianza muda mrefu uliopita na wananchi wa mataifa hayo mawili wamekuwa na ushirikiaano mkubwa katika masula ya Utamaduni kwa kushiriki katika Matamasha mbali mbali yanayoandaliwa na nchi hizo... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More