UGANDA YAFUZU TENA AFCON BAADA YA KUIPIGA CAPE VERDE 1-0 LEO NAMBOOLE - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

UGANDA YAFUZU TENA AFCON BAADA YA KUIPIGA CAPE VERDE 1-0 LEO NAMBOOLE

UGANDA imefuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa mara ya pili mfululizo, baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Cape Verde jioni ya leo Uwanja wa Mandela, Namboole mjini Kampala.
Ushindi huo unamaanisha Uganda, The Cranes wanafikisha pointi 13 baada ya kucheza mechi tano, ikishinda nne na sare moja na kumaliza kileleni mwa Kundi L nyuma ya Tanzania, yenye pointi tano, Cape Verde pointi nne na Lesotho pointi moja.
Lesotho watakuwa wenyeji wa Tanzania kesho Uwanja wa Setsoto mjini Maseru kabla ya kusafiri kwa mchezo wa mwisho na Cape Verde Machi mwakani, kipindi ambacho Uganda wataifuata Taifa Stars Dar es Salaam.

Katika mchezo wa leo, bao pekee la Uganda limefungwa na mshambuliaji wa KCCA ya nyumbani, Patrick Henry Kaddu dakika ya 78.
Hii inakuwa mara ya saba Uganda wanafuzu AFCON tangu walipofuzu mara ya kwanza mwaka 1962, huku matokeo mazuri zaidi kwao yakiwa ni ushindi wa pili katika fainali za mwaka 1978 baada ya kufungwa 2-0 na Uganda mabao ya Opoku Afriyie ‘Bayie’ dakika... Continue reading ->

Source: Bin ZuberyRead More