UHUSIANO KATI YA MWEKEZAJI NA WANANCHI WAIMARIKA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

UHUSIANO KATI YA MWEKEZAJI NA WANANCHI WAIMARIKA

Na Stella Kalinga, SimiyuWananchi na viongozi kutoka katika vijiji saba vinavyounda Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori (WMA) ya Makao hususani Kijiji cha Makao wilayani Meatu Mkoani Simiyu, wamekiri kuwa uhusiano kati yao na Mwekezaji MWIBA HOLDINGS LTD, ambaye amewekeza katika Hifadhi ya Wanyamapori ya MWIBA katika Kijiji cha Makao kwa ajili ya kuendeleza uhifadhi na uwindaji wa kitalii umeimarika tofauti na awali.
Hayo yalibainishwa na wananchi hao wakati wa ziara ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe.Anthony Mtaka na Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu, iliyoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa Enock Yakobo katika baadhi ya miradi na maeneo ya uwekezaji ya mwekezaji MWIBA HOLDINGS LTD  katika Hifadhi ya Wanyamapori ya MWIBA Kijiji cha Makao.
Wamesema awali kulikuwa na mgogoro ambao ulisababisha uhusiano kati wananchi na mwekezaji kuvunjika, lakini baadaye  Serikali ya Wilaya na Mkoa ziliingilia kati changamoto zote zilijadiliwa na mapunguf... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More