Ujenzi mradi wa umeme Rufiji kuanza mwezi Juni mwaka huu - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Ujenzi mradi wa umeme Rufiji kuanza mwezi Juni mwaka huu

Na Teresia Mhagama, PwaniImeelezwa kuwa ujenzi wa mradi wa umeme wa Rufiji utakaozalisha  megawati 2115 unatarajiwa kuanza rasmi tarehe 15 mwezi Juni mwaka huu. Hayo yalielezwa jana na Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani katika eneo utakapotekelezwa mradi huo wilayani Rufiji mkoani Pwani mara baada ya kukagua  kazi za ujenzi wa miundombinu wezeshi ya mradi huo ikiwemo barabara, umeme, maji na reli.
Katika ziara hiyo, Waziri wa Nishati aliambatana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constatine Kanyasu na Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa. Viongozi wengine walioshiriki ziara hiyo ni makatibu wakuu kutoka Wizara ya Nishati, Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Wizara ya Mifugo na uvuvi, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
Dkt. Kalemani alisema kuwa,  mkandarasi  ambaye ni Arab contractors amepewa miezi 36 ya ujenzi wa mradi huo na miezi sita ya ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More