UJENZI WA GATI NYAMISATI WAANZA, SHEHENA YA VIFAA YAANZA KUWASILI -KUANDIKWA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

UJENZI WA GATI NYAMISATI WAANZA, SHEHENA YA VIFAA YAANZA KUWASILI -KUANDIKWA


NA MWAMVUA MWINYI, KIBITI 

NAIBU waziri wa Ujenzi, Elias Kuandikwa amesema ujenzi wa gati, uliokuwa ukisubiriwa kwa kipindi kirefu na wakazi wa Nyamisati wilayani Kibiti mkoani Pwani umeanza ambapo shehena ya vifaa vya ujenzi vimeanza kuwasili tayari kwa ajili ya kazi. 

Aidha amewatoa wasiwasi wakazi wa Mafia kuhusu gati la Kilindoni ,kwamba linatarajiwa kuboreshwa kwa kuondoa dosari ndogondogo zilizopo ili liwe la kisasa. 

Akizungumza na wananchi wakati alipotembelea eneo litakapojengwa gati hilo, katika muendelezo wa ziara yake mkoani hapo, Kuandikwa alisema ujenzi utakuwa wa miaka miwili kwa gharama ya sh. bilioni 14 .

Alimtaka , mkandarasi wa gati hilo kufanya kazi inayotakiwa kwa kuhakikisha, ujenzi unakamilika kwa wakati ikiwezekana kuukamilisha kabla ya miezi 24.
Kuandikwa alisema, ujenzi umeshaanza na mkataba ulisainiwa tarehe 24,octoba mwaka huu, ombi lake ni kuona mkandarasi anamaliza kazi haraka.
“Fedha zipo hatutaki kuona mkandarasi anasuasua, gati litas... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More