UJENZI WA KIVUKO KIPYA CHA MV. MWANZA KUKAMILIKA MWEZI JUNI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

UJENZI WA KIVUKO KIPYA CHA MV. MWANZA KUKAMILIKA MWEZI JUNI

Na. Theresia Mwami - TEMESA
Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), imeahidi kukamilika kwa ujenzi kivuko kipya cha Kigongo Busisi (MV. MWANZA) unaofanywa kampuni ya kizalendo ya Songoro Marine Transport Boatyard ifikapo mwezi Juni 2018. Kivuko hicho kitakuwa na uwezo wa kubeba tani 250, ambazo ni sawa na kubeba magari 36 na abiria 1,000 kwa wakati mmoja.
Akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa kivuko hicho, uliofanywa na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya TEMESA mapema leo, Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Iddi Mgwatu alisema ujenzi huo unagharimu jumla ya shilingi za kitanzania bilioni 8.9 na ulianza rasmi tarehe 28/08/2017 na kwamba tayari umekamilika kwa asilimia 95.
“Namuagiza Mkandarasi kuhakikisha kuwa ujenzi wa kivuko hiki unakamilika kwa aslimia 100 ifikapo mwezi Juni,2018 kama ilivyoainishwa kwenye mkataba ili kuweza kuboresha zaidi huduma ya uvushaji abiria na mizigo yao katika eneo Kigongo – Busisi”, aliongeza Dkt. Mgwatu.
Ali... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More