Ujenzi wa uwanja wa Ndege wa Terminal 3 wakamilika kwa asilimia 81, kumalizika Mei 31 mwakani. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Ujenzi wa uwanja wa Ndege wa Terminal 3 wakamilika kwa asilimia 81, kumalizika Mei 31 mwakani.

Na Grace Semfuko- MAELEZO.
Ujenzi wa jengo la tatu la abiria katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar Es Salaam (Terminal 3) umekamilika kwa asilimia 81, na miezi minane ijayo kazi zote za ujenzi wa majengo na mahitaji yote ya uwanja yatakuwa yamekamiliki na tayari usafiri wa anga wa Tanzania kukidhi mahitaji yote ya kisasa kimataifa.
Ujenzi huo unaojengwa na kampuni ya Bam International ya Uholanzi ikisaidiwa na kampuni zingine 21 za kihandisi za ndani na nje ya nchi, ujenzi ulianza Juni mwaka 2013 na utakamilishwa Mei 31, 2019 kwa gharama Yuro 254 milioni, sawa na shilingi Bilioni 560 za kitanzania.
Akizungumza uwanjani hapo Msimamizi wa Jengo hilo kwa upande wa Mradi huo kutoka Wakala wa Taifa wa Barabara TANROADS, Mhandisi Burton Komba, amesema ujenzi huo unaendelea vizuri na kwamba kukamilika kwake kutarahisisha kusafirisha Abiria wa Kimataifa ambao kwa sasa wanahudumiwa na Uwanja huo jengo la pili (Terminal 2).
“Uwanja wa Ndege wa Kimataifa jengo la... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More