UJIO WA NDEGE AIRBUS 220-300 MAPOKEZI YAMEDAMSHI...SHANGWE TUPU UWANJANI,NDEGE KUTUA SAA 8:30 - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

UJIO WA NDEGE AIRBUS 220-300 MAPOKEZI YAMEDAMSHI...SHANGWE TUPU UWANJANI,NDEGE KUTUA SAA 8:30

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
SHANGWE,nderemo na vifijo vimetawala katika Uwanja wa Ndege jijini Dar es Salaam wakati wa Watanzania zaidi ya milioni 50 wakiangalia angani wakisubiri kuipokea ndege mpya ya Airbus 220-300 inayowasili leo mchana huu.
Mamia ya wananchi wamejitokeza kwa ajili ya kushuhudia ujio wa ndege hiyo ambapo pia viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwamo mawaziri wamewasili uwanjani hapo.
Kwa mujibu wa ratiba ambayo imetolewa kuhusu ujio wa ndege hiyo inaeleza kuwa  Rais Dk.John Magufuli atawasili uwanjani hapo saa nane kamili mchana.Na kabla ya hapo atawasili Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Baada ya viongozi hao kuwasili utaimbwa wimbo wa Taifa na kisha itafuata dua kutoka kwa viongozi wa dini  .Kwa mujibu wa ratiba itafuata hatua ya kutambulisha viongozi wa ngazi mbalimbali.
Itakapofika saa 8:30 hadi 8:40 ndege itawasili na kisha kupokea water Salute na baadae itafuata taarifa ya ndege.Saa 8:50 hadi 9:00 ndege itazinduliwa na baa... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More