Ujio wa Sevilla Fc ni fursa ya kukuza Michezo na Kuitangaza nchi: Shonza - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Ujio wa Sevilla Fc ni fursa ya kukuza Michezo na Kuitangaza nchi: Shonza

Na Shamimu Nyaki –WHUSMNaibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza amesema kuwa ujio wa timu ya Sevilla Fc kutoka Laliga nchini Hispania ni fursa kubwa ya kukuza na kuendeleza michezo hapa nchini.
Naibu Waziri ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati Kampuni ya SportPesa ilipotangaza ujio wa Klabu hiyo kubwa inayoshiriki ligi ya Laliga ikiwa nafasi ya tano ambayo inatarajiwa kuja nchini Mei 21 kucheza na mojawapo ya timu kubwa inayoshiriki ligi Kuu hapa nchini.“Ujio wa Sevvila Fc ni fursa kubwa sana kwa nchi yetu kwani itasaidia kutangaza na kuinua wachezaji na ligi yetu Ulimwenguni kote,”alisema Shonza.
Naye Waziri wa Maliasili na Utalii Hamisi Kingwangalla ameeleza kuwa ujio wa timu hiyo utachangia kutangaza utalii wa nchi yetu na ameahidi kuipeleka kutembelea moja ya hifadhi pamoja na kisiwa cha Zanzibar.Kwa upande wake Mkurugenzi na Mdhibiti wa Kampuni ya SportPesa Bw. Abbas Tarimba amesema Kampuni yake inaendelea kushirikiana na Serikali katika kuendeleza mic... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More