Ujumbe Makonda kwa Vijana wa Tanzania - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Ujumbe Makonda kwa Vijana wa Tanzania

Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ameweka picha yake ya zamani hii hapo chini na kuandika ujumbe kwa vijana wote wa kitanzania kuwa wasikate tamaa.

"Picha hii inanikumbusha safari yangu na mapambado niliyoyapitia. Kwa kifupi mwonekano huu ni tofauti sana na hali Na ndoto niliyokuwa nayo ndani yangu Kwa Mwonekano wa nje Nimedhoofika, nimechoka, mavazi hayaeleweki uso hauna tumaini na zaidi ya yote siwezi hata kumwaminisha mtu kuwa siku moja nitatimiza Ndoto zangu"- Makonda aliandika.

"Mwonekano huu unawakilisha idadi kubwa ya maisha ya vijana wa kitanzania ila ndoto yangu ilikuwa tofauti na mwonekano huo wa nje. Kwani ndani yangu nilikuwa na ndoto inayonisukuma kwenda mbele pamoja na upendo mkubwa wa Mungu. Nakuachia neno moja tu unapoanza wiki yako. USIKATISHWE TAMAA NA MWONEKANO WAKO, UNACHOTAKIWA NI KUAMINI KATIKA NDOTO ZAKO."- Makonda alimaliza.


Vijana tusikate tamaa.

... Continue reading ->
Source: Mwanaharakati MzalendoRead More