UJUMBE WA ROSTAM AZIZ KWA RAIS DKT. MAGUFULI BAADA YA KUTINGA IKULU - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

UJUMBE WA ROSTAM AZIZ KWA RAIS DKT. MAGUFULI BAADA YA KUTINGA IKULU

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
Mfanyabiashara maarufu nchini Rostam Aziz leo Novemba 13,2018 amekwenda kuonana na Rais Dk.John Magufuli ambapo ametumia nafasi hiyo kumpongeza Rais kwa utendaji kazi wake mzuri.Akizungumza mbele ya Rais Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam Rostam amasema “ Nimekuja kumuona Rais wangu na Mwenyekiti wangu wa Chama Cha Mapinduzi.“Nimekuja kumpongeza kwa kazi nzuri anazofanya, namtakia kila la kheri. Kama mfanyabiashara naona anachokifanya sasa Rais ni kutengeneza misingi ya uchumi utakaokuwa wa uhakika Zaidi,”amesema Rostam.
Ameongeza kuwa kwa lugha za kiuchumi ni kwamba Rais anatengeneza uwanja sawa katika kukuza uchumi na hilo ndilo jambo la msingi kwa kujenga uchumi imara.Pamoja na mambo mengine Rais Magufuli alimuuliza Rostam Aziz kama ni mshabiki wa Simba au Yanga ambapo alimjibu kuwa yeye ni Yanga.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mfanyabiashara Rostam Aziz Ikulu jijini Dar es Salaam.... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More