UJUMBE WA UAE WATEMBELEA MIRADI MBALI MBALI YA MAENDELEO MIKOA YA PEMBA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

UJUMBE WA UAE WATEMBELEA MIRADI MBALI MBALI YA MAENDELEO MIKOA YA PEMBA

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Abdalla Mzeee ya Mkoani Mkoa wa Kusine Pemba Dk.Haji Mwita (kushoto) akifuatana na  Ujumbe wa Timu ya Wataalam kutoka Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ulipofika kutembelea Hospitali hiyo leo kufuatia ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein aliyoifanya (UAE) mwanzoni mwa mwaka huu
Mkurugenzi Idara ya Tiba  DK.Mohamed Dahoma alipokuwa akitoa maelezo kwa ujumbe wa timu ya wataalamu kutoka katika  Serikali ya Umoja wa Nchi za Kiarabu (UAE) wakati ulipofika kutembelea katika Hospitali ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba leo,kufuatia ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika Nchi za UAE Mwanzoni kwa mwaka huu

 Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba Dk.Omar Issa(kushoto) alipokuwa akitoa maelezo kwa ujumbe wa timu ya wataalamu kutoka katika  Serikali ya Umoja wa Nchi za Kiarabu (UAE) wakati ulipofika kutembelea sehemu mbali mbali katika Hospitali ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba leo,kufuatia ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika Nchi za UAE Mwanzoni kwa mwaka huu Afisa Mdhamini katika Wizara ya Kazi,uwezeshaji,Wazee,Wanawake na Watoto Pemba Nd,Khadija Khamis Rajab (kushoto) alipokuwa akitoa maelezo kwa Mshauri wa Waziri wa Nchi Ushirikiano wa Kimataifa wa Serikali ya Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu (UAE)  Bibi Najla Al- Kaabi (katikati)akifuatana na ujumbe wa wataalamu kutoka Serikali ya Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu (UAE) uliotembelea kaaika Ushirika wa Wajasiriamali wa Kikundi cha Upendo Group Wete Pemba 
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji Nd.Shomari Omar Shomari (wa pili kulia)pamoja na Viongozi wengine wakimsikiliza Nd.Ali Humaid Alderei(kushoto) kutoka Mfuko wa Maendeleo wa (Abudhabi Fund) katika Ujumbe wa Timu ya Wataalam kutoka Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ulipofika kutembelea mradi wa Barabara ya Mkoani-Chakechake  Pemba leo kufuatia ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein aliyoifanya (UAE) mwanzoni mwa mwaka huuPicha na Ikulu.


Source: Issa MichuziRead More