UKAGUZI WA CAG KATIKA MASHIRIKA YA TBC NA TANESCO 2016/217 - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

UKAGUZI WA CAG KATIKA MASHIRIKA YA TBC NA TANESCO 2016/217

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) halijawahi kupata gawio kutokana na umiliki wa hisa 35 mtaji wa Star Media LTD tangu mwaka 2013 kwa sababu ya star Media kuripoti hasara ya sh.bilioni 61.
Akizungumza katika warsha ya Toleo Maalum kwa Wananchi na Kukusanya maoni kuhusu ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya mwaka 2016/2017 iliyofanyika Katika Ukumbi wa PPF Tower Mkaguzi wa Mashirika ya Umma Pascal Mahwago amesema kuwa star media iliripoti uchakavu wa vitu na kufanya TBC kukosa gawio licha ya kuwa na hisa.
Amesema kuwa ushauri wa CAG ulitaka kuhakikisha shughuli zote za kifedha zinafuatiliwa kwa ukaribu katika kuweza kupata gawio kutokana na uwekezaji wa hisa hizo.Kahwago amesema katika ukaguzi mwingine ni Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) lilikabidhi mali zisizohamishika kwa kampuni ya kufua umeme ya Songas mwaka 2004 zilizokuwa ndani ya Ubungo Complex kwa kupewa hisa 10,000 bila ya kukokotoa thamani halisi ya Mali walizokabidhi... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More