UKEREWE: Upanuzi Kituo cha afya Bwisya kisiwani Ukara wafikia asilimia 95 - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

UKEREWE: Upanuzi Kituo cha afya Bwisya kisiwani Ukara wafikia asilimia 95

Na George Binagi-GB Pazzo, BMGMkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella leo Ijumaa Juni 07, 2019 amekagua maendeleo ya upanuzi na ujenzi wa Kituo cha Afya Bwisya kilichopo wilayani Ukerewe na kulidhishwa na ujenzi wake ambao umefikia asilimia 95 kwa mujibu wa mkandarasi.
Upanuzi wa Kituo hicho kwa hadhi ya Hospitali ni sehemu ya agizo la Rais Dkt. John Pombe Maguli alilolitoa baada ya ajali ya Kivuko cha MV. Nyerere iliyotokea Septemba 20, 2018 ambapo alielekeza sehemu ya fedha za rambirambi ya ajali hiyo (Milioni 800) zitumike kufanya shughuli hiyo.
Mongella amesema ukarabati huo ulipaswa kukamilika mwezi Machi mwaka huu lakini umechelewa kutokana na changamoto ya miundombinu ya usafiri kwani baadhi ya vifaa ujenzi vinatoka jijini Mwanza na kusafirisha kwa njia ya maji hivyo matarajioni ni mkandarasi kampuni ya Suma JKT kukamilisha kazi hiyo mwishoni mwa mwezi huu.
Pia amekagua maendeleo ya Shule ya Sekondari Nyamanga iliyopo kisiwani Ukara aliyoiwekea jiwe la msingi la ujenzi Mei 02, 2019 na k... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More