ULEGA AFUNGUA RASMI MAONESHO YA NNE YA NDEGE WAFUGWAO NCHINI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

ULEGA AFUNGUA RASMI MAONESHO YA NNE YA NDEGE WAFUGWAO NCHINI

Na Leandra Gabriel, blogu ya jamii
NAIBU Waziri wa kilimo na uvuvi na Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega amezindua rasmi maonesho ya nne ya ndege wafugwao katika viwanja vya maonesho (sabasaba) jijini Dar es salaam.
Akizungumza katika uzinduzi huo Ulega ameeleza kuwa maonesho ya mwaka huu yamehusisha makampuni mengi ya ndani na nje ya nchi kama Kenya, Poland na China na amewakaribisha kuwekeza nchini kutokana na kuwepo kwa fursa za uwekezaji katika sekta mbalimbali.
Aidha ametoa pongezi kwa vyama vyote vya wadau wa ndege wafugwao chini ya chama mama cha Tanzania Poultry show (TPS) kwa kutoa kipaumbele katika suala la ufugaji wa kuku.Pia amewataka kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja  na wao kama serikali wapo pamoja kama walezi wao, katika kuhakikisha wanasonga mbele zaidi na amewapongeza kwa ushirikiano wao kupitia vyama vyao.
Ulega amesema kuwa Rais Magufuli ameendelea kusimamia maendeleo ambapo hadi sasa tozo zilizokuwa kero kwa wafugaji, wakulima na wavuvi zimeondolewa ili kuweza ku... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More