ULEGA ATATUA CHANGAMOTO YA DARAJA KITONGOJI CHA CHURWI KATA YA TAMBANI, MKURANGA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

ULEGA ATATUA CHANGAMOTO YA DARAJA KITONGOJI CHA CHURWI KATA YA TAMBANI, MKURANGA

MBUNGE wa jimbo la Mkuranga Mkoani  Pwani na  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega  ametembelea katika Kitongoji cha  Churwi, Kata ya Tambani na kukaguwa mradi wa kivuko ambapo amefanikiwa kutatua changamoto  ya kivuko hicho chenye historia ya kuuwa watoto wawili.
Akizungumza na wananchi wa eneo hilo, Ulega alisema kuwa ameridhishwa na kitendo cha wananchi kuweza kujichangisha na kuanza ujenzi wa kivuko ili kukabiliana na changamoto zilizokuwa zikiwakabili za kukosa kivuko kwa muda  wa miaka mingi.


Katika hali hiyo  imempelekea Naibu waziri huyo kuchangia mifuko ya saruji 60  na milioni moja na nusu  kuongeza nguvu katika ujenzi wa kivuko hicho.

Aidha  amewataka wananchi hao  kuongeza ushirikiano zaidi katika masuala  ya maendeleo kwani wananchi wanapoanzisha miradi ya maendeleo serikali  ni lazima iweke mkono  wake ili kuongeza nguvu.


"Tushirikiane ili kuokoa maisha ya watoto wetu  pia kivuko hiki  kitasaidia kufungua fursa  mbalimbali za maendeleo kutokana na ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More