ULEGA AWAASA WANA-CCM MKURANGA KUUSEMEA UTEKELEZAJI WA ILANI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

ULEGA AWAASA WANA-CCM MKURANGA KUUSEMEA UTEKELEZAJI WA ILANI

Na Mwamvua Mwinyi, Mkuranga  Mbunge wa Jimbo la Mkuranga ,Abdallah Ulega, amesema anaandaa mpango mkakati utakaowezesha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kushinda kwa kishindo katika chaguzi za serikali za mitaa 2019 na uchaguzi mkuu 2020.  Aidha amewatoa shaka wanaCCM wilayani hapo kwa kudai ushindi utapatikana kwani ahadi na ilani ya CCM inatekelezwa hivyo wapinzani hawana pa kupenya. Ulega ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, aliyasema hayo wakati akiongea na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Mkuranga .  Alisema, chama kipo imara na halmashauri kuu ya CCM wilaya ndiyo jeshi namba moja la kuhakikisha ushindi huo unapatikana katika chaguzi hizo.  "Msikae kimya ,kila mwanachama na kiongozi kuanzia ngazi za chini ni jukumu letu kushirikiana kuyasema mazuri yanayofanywa na serikali yetu na utekelezaji wa ilani"alisema.  Ulega alisisitiza umoja na ushikamano na kuacha kuyapa nafasi makundi ambayo hayana tija katika mustakabali wa kukiimarisha chama hicho. Alieleza a... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More