ULEGA AZIDI KUWAKUNA WAPIGA KURA WAKE,ACHANGIA UJENZI WA SHULE NA ZAHANATI MKURANGA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

ULEGA AZIDI KUWAKUNA WAPIGA KURA WAKE,ACHANGIA UJENZI WA SHULE NA ZAHANATI MKURANGA

Na Leandra Gabriel, Glogu ya jamii
NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amechagia kiasi cha shilingi milioni 4.7 katika kata ya Nyamato, mifuko 250 ya Saruji kwaajili ya ujenzi wa vituo vya afya, shule na nyumba za Wauguzi hii ni katika kuhakikisha huduma za elimu na afya zinaimarika na kuwa faafu kwa wananchi wote wa Mkuranga.
Wakati huo huo Ulega pia ametoa amechangia shilingi laki sita kwaajili ya ujenzi wa ofisi ya CCM Kata ya Kimanzichana na ameahidi kutoa kiasi cha milioni 2 kwaajili ya vikundi vya wanawake wajasiriamali.
Akizungumza wakati wa utoaji wa mchango huo Ulega ameeleza kuwa ushirikiano wa wananchi unampa nguvu ya kufanya makubwa zaidi katika kuleta maendeleo na amewataka watendaji kufuata kasi iliyopo na kumuunga mkono Rais John Magufuli kwa juhudi anazoonesha katika kuleta maendeleo nchini.
Pia Ulega amesema kuwa yupo pamoja na wananchi wa Mkuranga wakati wote na katika kufanya kila jambo litakaloleta maendeleo bila kujali itikadi wala chama.Katibu wa CCM Wi... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More