Ulipofikia mchakato mzima wa michuano mipya ya UEFA - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Ulipofikia mchakato mzima wa michuano mipya ya UEFA

Uefa kunani tena?


Bodi ya wataalamu wa soka wakisaidiana na UEFA wamekubaliana kwa moyo wa dhati kabisa kuongeza mashindano mengine. Hayao mashindano yatakwenda sambamba na Ligi ya Mabingwa pamoja na ligi ndogo ya ulaya maarufu kama Yuropa.Swali ni Je yataendeshwaje? Kwa mfumo upi?


Barnabas Gwakisa a.k.a Mr Darajani ambaye ni mmoja wa mashabiki damu dam wa Chelsea wamejiuliza maswali mengi kuhusiana na mashindano hayo. Mashabiki wengi pia wamekua na sintofaham juu ya sakata hilo.Michuano hiyo itaanza lini?


Michuano hiyo inatarajiwa kutimua vumbi msimu wa 2021-2022.


Je itashirkisa vilabu vingapi?


Michuano hii itajumuisha vilabu 32 kisha zitatengwa kwenye mfumo wa makundi makundi.


Je kuna athari zozote?


Mr Darajani anafahamu wazi kuwa utaratibu huu utakwenda sambamba na mabadiliko makubwa ya idadi ya vilabu vitakavyoshiriki Uefa na Yuropa.Kivipi?


Kuanzishwa kwa michuano hii kutapunguza timu zitakazoingia ligi ya Ulaya yaani Europa League kupungua kutoka timu 48 hadi kufikia 32, na hii inamaanisha kuwa makundi yatapungua hadi kufikia nane sawa na michuano ya klabu bingwa barani Ulaya (UEFA Champions League)Mabadiliko mengine je?


Lakini pia kutambulishwa ka michuano hii mipya kutabadilisha idadi ya vilabu vitakavyoshiriki michuano yote ya ulaya kutoka 80 hadi timu 96.


32 zitakuwa za Klabu bingwa barani Ulaya maarufu kama UEFA Champions League.
32 zitashiriki Ligi ya Ulaya maarufu kama Europa League.
32 zitashiriki michuano hiyo mipya.

Kuhusiana na mchakato wa uendeshwaji wa michuano hiyo bado ni kitendaliwi na shirikisho la soka barani ulaya wanaendelea kufanya mazungumzo ili kung’amua mchakato mzima wa uratibishaji wa michuano hiyo.Yondani fiti kuikabili Stand United kutazama video bonyeza hapaMr Darajani pia hakuacha kutoa mawazo na msimamo wake juu ya sababu kubwa kwa maandalizi ya michuano hii.


“Moja ya sababu ambayo naiona imefanya kuundwa kwa michuano hii ni ili kuzidi kuongeza wawekezaji na udhamini na kuzidi kuzivutia chaneli za televisheni kuzidi kuwekeza katika soka la barani Ulaya”“Ni kama walivyoeleza sababu ya kuamua kuanzisha michuano ya ligi ya timu za taifa (UEFA Nations League) ambapo walisema wameamua kuianzisha ligi hiyo ya timu za taifa ili kuzidisha thamani ya michezo hiyo na kuitoa katika mtindo wa michezo ya kirafiki. Kwa hivyo kubwa walilolinlenga katika michuano hii ni sababu za kibiashara na udhamini”


Kwingineko shirikisho la soka barani Ulaya lipo kwenye mchakato mwingine wa kujaribu kuangalia uwezekano wa fainali ya klabu bingwa Barani Ulaya kuchezwa nje ya Bara la Ulaya.Marekani inatajwa zaidi kama taifa ambalo lina fursa nzuri ya kupata nafasi hiyo. Majiji ya kadhaa ya Marekani yanatarajia kutuma zabuni hiyo huku Miami ikitajwa kuwa na mji unaowania kwa udi na uvumba kuandaa fainali hizo.


Source: Shaffih DaudaRead More