UMOJA WA MAKANISA YA KIPENTECOSTE SHINYANGA WAFANYA MAZOEZI, WACHANGIA DAMU SALAMA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

UMOJA WA MAKANISA YA KIPENTECOSTE SHINYANGA WAFANYA MAZOEZI, WACHANGIA DAMU SALAMA

Umoja wa makanisa ya Kipentecoste Mkoani Shinyanga wamefanya mazoezi na kuchangia damu salama, ili kuunga juhudi za Serikali ya awamu ya tano kwa kuimarisha afya za wananchi, pamoja na kuokoa vifo vya mama na mtoto vitokanavyo na uzazi kwa sababu ya kumwaga damu nyingi.
Mazoezi hayo yamefanyika leo Juni 15, 2019 kwenye uwanja wa wamichezo wa Sabasaba, na kuongozwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga, mhe. Jasinta Mboneko, ambayo yalianza kwa matembezi na kukimbia kwa kuzunguka mji wa Shinyanga na kuhitimishwa kwa kuchangia damu salama. Akizungumza kwenye mazoezi hayo, mwenyekiti wa umoja wa makanisa hayo ya Kipentecoste mkoa wa Shinyanga,Askofu Elias Madoshi, amesema wao kama viongozi wa kidini wameona ni vyema kuunga juhudi za Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli, kwa kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi pamoja na kuchangia damu salama. 
Amesema juhudi za serikali ya awamu ya tano zinapaswa kuungwa mkono, ambapo wananchi wakiwa na afya mgogoro kamwe hawataweza... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More