UMOJA WA MASHABIKI WAIFUTURISHA TIMU YAO NA KUTOA UJUMBE MZITO KWA UONGOZI WA TIMU - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

UMOJA WA MASHABIKI WAIFUTURISHA TIMU YAO NA KUTOA UJUMBE MZITO KWA UONGOZI WA TIMU

Bukoba na Allawi Kaboyo.Umoja wa mashabiki wa timu ya soka ya  Kagera Sugar inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara wameiandalia timu hiyo futari iliyowajumuisha wachezaji wote wa timu hiyo,benchi la ufundi, viongozi wa timu pamoja na mashabiki ikiwa ni ishara ya kuonesha umoja na upendo kwa timu yao.
Futari hiyo iliandaliwa jana tarehe 16 mwezi machi mwaka huu  katika ukumbi wa Red Cross Bukoba mkoani Kagera na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa kiserikali na dini katika kuonesha mshikamano baina ya mashabiki na timu.
Akiongea mmoja wa viongozi wa umoja wa mashabiki ambaye ni katibu  wa jumuiya hiyo ndugu Alex Xavery aliutaka uongozi wa timu ya Kagera sugar kuonesha ushirikiano na mashabiki ili kuweza kuijenga timu lakini pia kuwafanya mashabiki kuwa karibu zaidi na timu yao. Katibu huyo aliongeza kuwa timu kwa sasa ina hali mbaya katika msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara kutokana na kutofanya vizuri katika msimu huu ambapo alimuomba mwalimu wa timu hiyo Meck Maxime kuwa na malengo y... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More