UNAHITAJI KUPIMIWA ARDHI ?, UTARATIBU NI HUU. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

UNAHITAJI KUPIMIWA ARDHI ?, UTARATIBU NI HUU.

Na Bashir Yakub.
Ardhi iwe kiwanja au nyumba thamani yake hupanda pale inapokuwa imepimwa. Kupima ardhi ni kurasimisha ardhi. Faida nyingi hupatikana baada ya ardhi kuwa imerasimishwa. Baadhi ya faida ni kuwa ardhi hupanda thamani yake, kuweza kupata mkopo kwa urahisi, ardhi kutumika kama dhamana mahakamani, lakini kubwa ni kuwa na amani na uhakika wa ardhi yako kuwa eneo ulilopo linaruhusiwa kisheria, sio eneo hatarishi, sio eneo la miradi ya serikali, sio hifadhi ya barabara au barabara nk. Unakuwa na amani kuwa uko sehemu sahihi na salama. 
Kupima ardhi ni hatua inayopitiwa pale unapoelekea kupata hati. Kila ardhi yenye hati imepimwa lakini si kila ardhi iliyopimwa ina hati. 
UTRATIBU WA KUPIMIWA ARDHI. 
1.Kuandika barua ya maombi ni hatua ya kwanza ambapo utatakiwa kumwandikia mkurugenzi wa halmashauri ukiomba kupimiwa eneo lako. Hii ni barua ya kawaida ya kiofisi isipokuwa ieleze majina yako kwa ukamilifu na ichambue anuani ya eneo ambalo linalotakiwa kupimwa kwa ukamilifu.Mkur... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More