UNESCO waendesha kongamano la utawala kwa redio za jamii - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

UNESCO waendesha kongamano la utawala kwa redio za jamii

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limeendesha kongamano la siku tano lenye lengo la kufunza menejimenti, uongozi na utawala  kwa mtandao wa redio za jamii nchini (TADIO).Kongamano hilo limefanyika Jijini Dodoma kuanzia Julai 17 – 21 .Kwa mujibu wa UNESCO mafunzo hayo yamelenga kuimarisha mtandao huo.Mafunzo hayo yalifanywa kwa ajili ya watumishi muhimu wa radio hizo, bodi ya mtandao, sekretarieti ya mtandao na wawakiklishi wa radio wanachama.Lengo ni kusaidia redio hizo kutoa huduma zenye ubora wa hali ya juu.Mafunzo hayo yametokana na utafiti uliofanywa kuhusu menejimenti na uongozi wa TADIO katika utekelezaji wake wa majumumu hasa kufuatia malengo ya uwapo wa radio hizo.UNESCO ikisaidiwa na Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC) kwa ufadhili wa Empowering Local Radio kupitia tehama imetoa mafunzo hayo yenye lengo la kuinua ubora wa kazi za redio hizo.Mafunzo hayo ni sehemu ya mradi unaowezesha redio 25 za kijamii zilizo wanachama wa TADIO kuhakikish... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More