UNHCR: Watu milioni 70.8 wanaishi kama wakimbizi duniani - Kwanza TV | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

UNHCR: Watu milioni 70.8 wanaishi kama wakimbizi duniani

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia  Wakimbizi, UNHCR limesema watu takriban milioni 71 wameyakimbia makazi yao duniani kote, kuepuka ghasia na unyanyasaji. Miongoni mwao milioni 41 ni wakimbizi wa ndani ya nchi zao.


Ripoti hiyo ya UNHCR imetangazwa kwenye mkesha wa siku ya kimataifa kwa ajili ya wakimbizi ambayo inaadhimishwa kesho Alhamis. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, watu milioni 70.8 walilazimika kuyahama makazi yao mwaka uliopita, hilo likiwa ongezeko la watu karibu milioni mbili ikilinganishwa na mwaka uliotangulia.


Akiizindua ripoti hiyo mapema leo mjini Geneva, Kamishna wa UNHCR  Filippo Grandi, amesema kwa bahati mbaya hali inachukua mwelekeo usio sahihi, na kwamba imeibuka mizozo mipya ambayo inaongeza idadi ya wakimbizi ya waliopo sasa. Grand amepinga dhana kwamba wote wanaozihama nchi zao ni wakimbizi wa kimaslahi.


”Watu huyahama makazi yao kwa sababu mbalimbali, ambazo tunaweza kuziita za mseto. Bila shaka, wapo wanaoondoka kutafuta fursa bora za kiuchumi, laki... Continue reading ->


Source: Kwanza TVRead More