Uongo Wakwamisha Penzi la Ben Pol na Ebitoke. - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Uongo Wakwamisha Penzi la Ben Pol na Ebitoke.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye ilisemekana yupo kwenye mahusiano ya kimapenzi na muigizaji wa vichekesho Ebitoke, ameweka wazi juu ya mahusiano yao kwamba walishindwa kuwa wapenzi kutokana na mmoja wao kutokuwa muwazi kwa mwenzake.


Ben Pol amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara kupitia ukurasa wa kijamii wa facebook wa EATV, baada ya miongoni mwa shabiki zake waliokuwa wakimfuatilia, alipotaka kufahamu undani wa mahusiano yake na Ebitoke.


“Kiukweli sijawahi kuwa na mahusiano na Ebitoke na wala ile haikuwa kiki. Kilichotokea ni kwamba hatukufanikiwa kuwa na mahusiano licha ya wananchi au mashabiki zangu wenyewe kumpitisha kuwa mpenzi wangu kabla ya mimi sijamuona na kumkubali”, amesema Ben Pol.


Pamoja na hayo, Ben Pol ameendelea kwa kusema “Ebitoke alikubarika hadi kwa wazazi wangu kutokana na yeye kuonekana kwenye vyombo vya habari akidai mimi ni mpenzi wake. Wazazi wakawa wanajua kwamba wameshapata mkwe wao. H... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More