Uongozi Wizara ya Viwanda Wawatoa Hofu Wakulima wa Korosho - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Uongozi Wizara ya Viwanda Wawatoa Hofu Wakulima wa Korosho

Kuhakikisha azma ya Serikali ya Awamu ya Tano inanunua korosho yote ya wakulima inatimia kabla ya kipindi cha masika hakijashika kasi, uongozi wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji umewatoa hofu wakulima wote wa mikoa ya kusini kuwa serikali inao uwezo wa kununua na kihifadhi korosho yote itakayonunuliwa.
Hakikisho hilo limetolewa na Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph Buchwaishaija wakati anahitimisha siku ya kwanza ya oparehseni ya ukaguzi wa maghala kwenye mikoa ya Lindi na Mtwara. “Ziara ya ukaguzi wa maghala inatokana maagizo ya kikao cha tathmini ya Operesheni Korosho kilichoitishwa na Mwenyekiti wake Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga, ambapo pamoja na mambo mengine kilibaini ufinyu wa maeneo ya kuhifadhia korosho kutoka kwa wakulima” anasema Prof. Buchweishaija. 
Kwenye ziara hiyo Prof. Buchwaishaija pamoja na Naibu Katibu Mkuu (Viwanda) Ludovick Nduhiye na maafisa wengine waandamizi wa wizara hiyo walifanikiwa kukagua maghala ya kor... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More