UPANDE WA MASHTAKA WAPEWA SIKU SABA KUKAMILISHA MCHAKATO KUBADILI HATI YA MASHTAKA KESI YA AKINA AVEVA, NYANGE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

UPANDE WA MASHTAKA WAPEWA SIKU SABA KUKAMILISHA MCHAKATO KUBADILI HATI YA MASHTAKA KESI YA AKINA AVEVA, NYANGE

Na Ripota Wetu,Globu ya jamii
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa siku saba kwa upande wa mashtaka kukamilisha mchakato wa kubadilisha hati ya mashtaka kwa kuwaondoa Zacharia Hans Poppe na Franklin Lauwo ili kesi dhidi ya washtakiwa Evans Aveva na Godfrey Nyange iweze kuendelea.
Amri hiyo, imetolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba baada ya Wakili wa Takukuru, Leonard Swai kueleza mahakamani hapo kesi imepangwa kwa ajili ya kutajwa na washtakiwa Aveva na Nyange wapo mahakamani.
Amedai mara ya mwisho Mahakama ilitoa agizo la kuwaondoa Poppe na Lauwo katika hati ya mashtaka ili kesi iendelee kwa Aveva na Nyange.Amedai utaratibu umefanyika na jalada limepelekwa kwa DPP na amejitahidi kulifuatilia hadi leo asubuhi na ametoka kwa DPP lakini hajaweza kulishughulikia, yupo nje ya Dar es Salaam.
Kutokana na hali hiyo ameomba Mahakama wapewe wiki mbili kwa ajili ya kuhakikisha DPP analifanyia kazi hata kama atakuwa Dodoma watamfuata huko huko.Baada ya Hakimu Swai kueleza hayo, Aveva alio... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More