UPANDE WA UTETEZI KESI YA 'UCHOCHEZI' INAYOWAKABILI VIONGOZI CHADEMA WATOA MAOMBI YAO ,WAWASILISHA MAPINGAMIZI NANE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

UPANDE WA UTETEZI KESI YA 'UCHOCHEZI' INAYOWAKABILI VIONGOZI CHADEMA WATOA MAOMBI YAO ,WAWASILISHA MAPINGAMIZI NANE

Na Karama Kenyynko,Blogu ya jamii
UPANDE wa utetezi katika kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi tisa wa Chadema akiwemo Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe, wameomba Mahakama kutupilia mbali mashtaka dhidi ya washtakiwa kwa kuwa yanamapungufu, kisheria.
Maombi hayo yamewasilishwa leo mahakamani hapo  mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Wilabard Mashauri wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Wakili Peter Kibatala.Hivyo amewasilisha mapingamizi nane ya kisheria yanayoshambulia uhalali wa hati ya mashtaka na mashtaka dhidi ya washtakiwa.
Katika mapingamizi hayo, Kibatala amedai, kibali cha DPP kina mapungufu ya kisheria kwa sababu haioneshi imetolewa kwa mashtaka yapi  na pia hati ya mashtaka imewataja majina washtakiwa wote bila ya kufafanua na pia imetaja tu kifungu cha sheria ambacho washtakiwa wameshtakiwa nacho Amedai, hakuna kibali kilichowasilishwa mahakamani hapo kwa maana hiyo mashtaka dhidi ya washtakiwa yamepelekwa mahakamani hapo bila ridhaa ya DPP.Amedai Aidha Kibatala ametoa ombi mbadala na kuomba, iwapo Mahakama itashindwa kuifuta hati nzima ya mashtaka yanayowakabili washtakiwa hao basi iyafutilie mbali mashtaka ambayo yanamapungufu kisheria. Ikiwamo shtaka la nne, latano, la sita na la saba.
Alidai, maelezo ya mashtaka hayo yanawachanganya washtakiwa na hawawezi kujitetea ipasavyo. Pia mashtaka hayo kufunguliwa kwake kunahitaji ridhaa ya (DPP) ambayo haipo kutokana na mapungufu hayo, inaonesha hakuna ridhaa yake.
Amebainisha kwa kuwa mashtaka hayo tajwa kufunguliwa kwake kunahitaji ridhaa ya DPP, lakini kuwa haipo tunaomba yafutiliwe mbali. Alidai Kibatala.Pia alidai hati ya mashtaka inamapungufu kwa sababu shtaka la pili na la Tatu hayana maelezo ya kutosheleza ya kuwapa washtakiwa msingi na uwezo wa kuweza kujitetea kikamilifu katika kesi hiyo ya jinai.
Alidai, katika shtaka la kufanya mkusanyiko bila kibali hati haijataja watu waliotishiwa na wametajwa kwa wingi hivyo haijulikani ni washtakiwa ama ni watu wengine.
Akiendelea kuwasilisha maoungamizi hayo, kibatala amedai, mashtaka yanayowakabili washtakiwa hao yamejichanganya na hayaonyeshi walipelekeaje kifo cha Akwilina na hao majeruhi walijeruhiwa na nani na kwa kutumia nini.
KUSOMA ZAIDI BOFYA 


Source: Issa MichuziRead More