UPATIKANAJI WA NAKALA ZA HUKUMU NA NYARAKA NYINGINE ZA MAHAKAMA WABORESHWA ZAIDI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

UPATIKANAJI WA NAKALA ZA HUKUMU NA NYARAKA NYINGINE ZA MAHAKAMA WABORESHWA ZAIDI

Na Mary Gwera, Mahakama ya TanzaniaMahakama ya Tanzania iliingia mkataba na Shirika la Posta kuhakikisha kuwa huduma ya kusambaza nyaraka mbalimbali za Mahakama inatolewa kwa nchi nzima. Mkataba huu chini ya huduma mpya ya Posta mlangoni (The post at your door step) iliyoanzishwa na Shirika la Posta, umelipa jukumu la kukusanya na kusafirisha/kusambaza nakala za hukumu na nyaraka mbalimbali za Mahakama na kuzifikisha kwa wahusika kulingana na anuani zao na mahali walipo (Anuani za makazi).
Kwa kipindi kirefu kumekuwa na malalamiko miongoni mwa wananchi/wateja wa Mahakama juu ya usumbufu katika upatikanaji wa Nakala za hukumu na baadhi ya nyaraka za Mahakama, hali ambayo kwa namna moja au nyingine ilisababishwa kwa kutokuwa na taarifa sahihi za Mdaawa/Mteja na utaratibu stahiki wa ufikishaji wa nyaraka hizo. Mahakama ya Tanzania katika utekelezaji wake wa majukumu mbalimbali inawalenga wateja wake ili kuhakikisha haki inatolewa kwa wakati na kuimarisha imani ya Wadau kwa Mahakama. Utoaji wa... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More