UPELELEZI KESI YA AMBER RUTTY NA MUMEWE WAKAMILIKA, KUUNGURUMA MARCH 07 - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

UPELELEZI KESI YA AMBER RUTTY NA MUMEWE WAKAMILIKA, KUUNGURUMA MARCH 07

 Upelelezi katika kesi ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile inayomkabili msanii Rutyfiya Aboubakary maarufu Kama Amber Rutty na mume wake Said Mtopali umekamilika na sasa kesi hiyo itaanza kuunguruma Machi 7 kwa washtakiwa hao kusomewa maelezo ya awali.
Wakili wa Serikali, Faraji Nguka ameeleza hayo leo Februari 11.2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustine Rwizile wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.Wakili Nguka amedai, kesi hiyo leo imekuja kwa kutajwa lakini upelelezi umekamilika, hivyo wanaomba tarehe kwa ajili ya kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali. Kufuatia taarifa hiyo,  Hakimu Rwizile ameahirisha kesi hiyo hadi March 7, 2019. Amber Rutty na mumewe walifikishwa mahakamani hapo November 2, 2018 wakikabiliwa na kosa la kufanya mapenzi kinyume na maumbile.
Mbali na wawili hao, mshtakiwa mwingine ni James Charles maarufu kama ‘James Delicious’.
Katika kesi hiyo kosa la kufanya mapenzi kinyume na maumbile linamkabili Amber Ruth, ambapo anadaiwa amelitenda kati ama baada ya... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More