UPELELEZI KESI YA KITILYA NA WENZAKE BADO HAUJAKAMILIKA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

UPELELEZI KESI YA KITILYA NA WENZAKE BADO HAUJAKAMILIKA

Na Karama Kenyunko blogu ya Jamii.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa na upande wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili,  aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya na wenzake kuwa wanawasiliana na wachunguzi ili wajue upelelezi umefikia wapi.
Mbali na Kitilya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kampuni inayoshughulikia  Uwekezaji wa Mitaji na Dhamana (Egma), washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa Miss Tanzania (1996), Shose Sinare na Ofisa wa benki ya Stanbic, Sioi Solomon.
Wakili wa Serikali, Patrick Mwita ameeleza hayo leo Novemba 9.2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati kesi dhidi ya washtakiwa hao ilipoletwa kwa ajili ya kutajwa. Wakili Mwita amedai upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika, bado wanaendelea kuwasiliana na wachunguzi.Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 16, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na kuangalia kama upelelezi umekamilika ama la.Washitakiwa wote kwa pamoja  wanakabiliwa na mashitaka ya... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More