URUSI: Ndege yatua kwenye shamba la mahindi baada ya kuvamiwa na kundi la ndege - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

URUSI: Ndege yatua kwenye shamba la mahindi baada ya kuvamiwa na kundi la ndege

Ndege ya abiria ya Urusi imelazimika kutua kwa dharura kwneye shamba la mahindi karibu na jiji la Moscow baada ya kugonga kundi la ndege.Watu ishirikini na watatu wamejeruhiwa katika tukio hilo, ambalo limesababisha ndege kutua huku injini yake ikiwa imezima na gia yake kutua ikirudi nyuma, wamesema maafisa wa afya.


Ndege hiyo Ural Airlines Airbus 321 ilikuwa ikisafiri kuelekea katika eneo la Simferopol Crimea ilipogonga kundi la ndege muda mfupi baada ya kuondoka uwanjani , hali iliyovuruga utendaji wa injini yake.


Ndege ilikuwa na abiria 233 p na wahudumu ndani yake ilipolazimika kutua kwa dharura


Vyombo vya habari vya taifa la Urusi vimetaja kutua kwa ndege hiyo kama “muujiza wa eneo la Ramensk”.


Maafisa wa ndege hiyo wamesema ndege imeharibika sana na haiwezi kupaa tena. Uchunguzi rasmi juu ya ajali hiyo unaendelea.


Kwa mujibu wa mashirika ya habari ya  The Mosco TimesReuters na BBC, Ndege hiyo ilikwa na abiria 233 na wahudumu ndani yake wakati ndege waliporipotiwa kuingia ndani ya injini na rubani wake akaamua kutua mara moja.


Abiria mmoja ambaye hakut... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More