USAFIRI WA MWENDOKASI KUONGEZEWA MAGARI KUKIDHI HAJA ZA JIJI LA DAR ES SALAAM - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

USAFIRI WA MWENDOKASI KUONGEZEWA MAGARI KUKIDHI HAJA ZA JIJI LA DAR ES SALAAM


Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo ameagiza kuongezwa kwa mabasi 10 ya kawaida katika Usafiri wa Mwendokasi jijini Dar es Salaam ili kupunguza changamoto ya usafiri huo
Jafo alitoa agizo hilo jana jijini Dar es Salaam baada ya kufanya ziara katika kituo cha mwendokasi cha Kivukoni na kuzungumza na abiria kuhusu changamoto wanazokutana nazo katika usafiri huo wa mabasi ya mwendokasi.
Akizungumza na waandishi wa habari, Jafo alisema usafiri huo wa mwendokasi umekuwa ukisuasua jambo ambalo halimfurahishi ikizingatiwa kwamba wananchi wengi wamekuwa wakiutegemea.
Alisema tatizo hilo limekuwa likijitokeza mara kwa mara na kusababisha usumbufu kwa wananchi na mpaka sasa hajaona njia stahiki na ya kuridhisha zilizochukuliwa na watoa huduma katika kupata ufumbuzi changamoto hiyo.
“Tatizo hili limekuwa likijitokeza mara kwa mara katika kituo cha mabasi cha Kimara wakati wa asubuhi na Kivukoni na Gerezani wakati wa jioni. Imeonekana pia kuna w... Continue reading ->

Source: Mwanaharakati MzalendoRead More