USAID YAPONGEZA MCHANGO WA MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII-TASAF KATIKA KUBORESHA MAISHA YA WANANCHI. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

USAID YAPONGEZA MCHANGO WA MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII-TASAF KATIKA KUBORESHA MAISHA YA WANANCHI.

Na. Estom Sanga-TASAF 
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa -USAID, Andy Karas amefanya ziara katika mkoa wa Kagera na kukagua shughuli zinazofanywa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF na kuridhishwa na maendeleo yaliyofikiwa katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini mkoani humo.
Akiwa katika kijiji cha Mishenyi kata ya Butelankuzi wilaya ya Bukoba Vijijini ,Mkurugenzi Mkazi huyo wa USAID alitembelea Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambako alijionea namna Walengwa hao walivyoboresha makazi yao kwa kujenga nyumba bora kwa kutumia ruzuku itolewayo na TASAF .
Aidha Karas alipata ushuhuda wa Walengwa namna wanavyotumia ruzuku hiyo katika kuboresha huduma za elimu na afya kwa kaya zao huku pia wakitilia mkazo suala la uanzishwaji wa miradi midogo midogo ya uzalishaji mali kwa lengo la kujiongezea kipato chao.
“huu ni mwelekeo sahihi na unaopaswa kuungwa mkono na wapenda maendeleo kama USAID kwani unatekelezwa kwa misingi endelevu” alisi... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More