“Usajili wa mchezaji sio kama bidhaa sokoni”-Shaffih Dauda kuhusu Fei Toto - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

“Usajili wa mchezaji sio kama bidhaa sokoni”-Shaffih Dauda kuhusu Fei Toto

Usajili wa Fei Toto bado unaendelea kuchukua headlines kutokana na kutambulishwa na vilabu viwili tofauti (Singida United na Yanga).


Mambo kama haya yanatokea kwenye soka japo kwa wenzetu ni mara chache sana kuona mambo ya namna hii.


Tanzania kuna vitu ambavyo tunatakiwa kujifunza kwa wenzetu, tusiangalie vitu kwa jicho la taarifa au ushabiki pekee, bali vitu vinavyotokea kwa wenzetu waliopiga hatua kwenye michezo tuvilete kwetu na kuvifanyia kazi.


Tumejifunza nini huhusu uhamisho wa Ronaldo kutoka Madrid kwenda Juve?


Tulianza kusikia tetesi Cristiano Ronaldo anatakiwa na Juve na haikuwepo taarifa rasmi kwamba wanamsajili Ronald.


Baada ya tetesi ikaja taarifa kwamba Juve na Madrid wameongea juu ya Juve kutaka kumsajili Ronaldo, wamekubaliana na Madrid wakairuhusu Juve ikazungumze na mchezaji akikubali warudi tena kwa uongozi wa Madrid.


Juve wakazungumza na Ronaldo, akawapa mahitaji yake na masharti wakakubaliana. Juve wakarudi kwa Madrid kuripoti kwamba wameshakubaliana na mchezaji.


Ma... Continue reading ->


Source: Shaffih DaudaRead More