USHAWISHI KUMPANGA BOSI - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

USHAWISHI KUMPANGA BOSI

Juzi nilivutwa na ujumbe wa Mhe. Waziri January Makamba aloubandika kwenye kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Ujumbe ule ukiwalenga wateule wapya wa Mh. Rais Dr. J.P.J. Magufuli akiwaasa baadhi ya mambo ya kuepuka "the don'ts" kwenye nafasi hizo mpya za utumishi wenye mamlaka.
"Usikubali mtu akakubebea mkoba"
"Usikubali mtu akakupakulia chakula kama mnakula kwenye bufee"
Ingawa naweza kuwa sijanukuu kwa usahihi wake, hayo mawili ni baadhi ya mambo aliyoandika waziri Makamba akiwaambia wateule hao ambao katika andiko lake aliwaita "wadogo zangu"
Ni jambo la kupendeza haswaa kunapotokea mtu mzoefu kwenye nafasi za uteuzi kutumia muda wake kuwakumbusha wateule wapya mambo madogomadogo kama hayo ambayo kimsingi huwa ni kero ambayo mtu hawezi kusema.
Binadamu tumeumbwa na akili za ajabu sasa, nadhani mtu anapokuwa kiongozi kuna mambo anakosa fursa ya kuyaona kuwa si mema.
Na kwa kuwa ni kiongozi tayari na anamamlaka ya uongozi huo, nadhani pia hukosa fursa nyingine ya kumpata mtu wa kawaida wa kumwambia hiki... Continue reading ->


Source: KajunasonRead More