USHIRIKI WA TANZANIA KATIKA SIKU YA USAFI DUNIANI WAFANA - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

USHIRIKI WA TANZANIA KATIKA SIKU YA USAFI DUNIANI WAFANA

Mkurugenzi wa Taasisi ya Nipe Fagio, Ana Rocha akielezea matokeo ya siku ya usafi duniani iliyofanyika hivi karibuni katika mikoa mbali mbali ya Tanzania. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
*Maelfu wajitokeza kushiriki nchi nzima*Dar es Salaam yabainika kuwa eneo lililochafuliwa zaidi
Zaidi ya watu elfu ishirini na sita walijitolea kushiriki kwenye Siku ya Usafi Duniani ya kwanza na kukusanya zaidi ya tani mia nne za taka kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Kwa mujibu wa Ana Rocha, Mkurugenzi wa Taasisi ya Nipe Fagio walioratibu tukio hilo nchini watu 26,419 walijitokeza kushiriki Siku ya Usafi Duniani katika maeneo mbalimbali ya nchi na kukusanya jumla ya kilo 466,378 za uchafu sehemu kubwa ikiwa ni plastiki zitokananzo na vifungashio vya chakula na vinywaji.
Amesema jiji la Dar es salaam ndio mkoa ambao umeathirika zaidi na uchafu nchini. Taka nyingi zaidi zilizokusanywa kwenye Siku ya Usafi Duniani zilitoka maeneo ya Buza Majumba 3 wilaya ya Temeke... Continue reading ->


Source: KajunasonRead More