USHIRIKIANO SEKTA YA UMMA NA SEKTA BINAFSI KUIBUA MIRADI YA KIMKAKATI KUKUZA UCHUMI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

USHIRIKIANO SEKTA YA UMMA NA SEKTA BINAFSI KUIBUA MIRADI YA KIMKAKATI KUKUZA UCHUMI


Na Mwandishi Maalum, Tanga

Serikali imezitaka Wizara na Taasisi za Umma kuhakikisha zinawajibika kikamilifu kufuata hatua zote muhimu za utekelezaji wa miradi ya Ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi (Public Private Partinaship-PPP), kwa kuwa hatua hiyo itaiwezesha Serikali kupata miradi ya maendeleo yenye sifa na ubora unaotakiwa nchini.

Hayo yameelezwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Mhandisi Zena Said alipokuwa akifungua mafunzo ya siku tano ya ubia kati ya Sekta za Umma na Sekta Binafsi (PPP) kwa Maafisa wa Wizara ya Fedha na Mipango, Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) , Taasisi na Mashirika ya Umma nchini.

Alisema kuwa utaratibu huo wa PPP ni njia bora ya kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo ile ya kibajeti na kuiwezesha Serikali kuweza kufikia malengo yake katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo na kutoa huduma bora na zenye tija kwa wananchi wake. 

Mhandisi Zena aliongeza kuwa, iwapo Halmashauri nchini zi... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More