USHIRIKIANO WA TAASISI ZA DINI NA SERIKALI NI MUHIMU-MAJALIWA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

USHIRIKIANO WA TAASISI ZA DINI NA SERIKALI NI MUHIMU-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ushirikiano mzuri baina ya taasisi mbalimbali za dini nchini na Serikali ni jambo la muhimu katika kuboresha na kuimarisha amani.
Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Oktoba 22, 2018) alipowasili jijini Mwanza akiwa njiani kwenda mkoani Simiyu ambako kesho anatarajia kufungua maonesho ya wajasiriamali.Alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza, Waziri Mkuu amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella na viongozi mbalimbali wa mkoa huo wakiwemo wa Serikali na wa dini mbalimbali.
Waziri Mkuu amesema Serikali inatambua mkakati wa viongozi wa dini wa kuunda kamati za amani nchini ambapo walianzia kwenye ngazi ya mkoa na sasa wamefikia katika kata.“Viongozi wa dini mnadhamana kubwa katika kulifanya Taifa liendelee kudumisha amani, utulivu na mshikamano, hivyo ushirikiano wenu na Serikali ni muhimu.”
Amesema viongozi wa Serikali wakati wote wamekuwa tayari kufanyakazi na viongozi pamoja na taasisi mbalimbali za dini, lengo ni kuimarisha amani na utu... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More