USIKATISHWE TAMAA, SONGA MBELE CHANGAMOTO NI HATUA KATIKA MAISHA - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

USIKATISHWE TAMAA, SONGA MBELE CHANGAMOTO NI HATUA KATIKA MAISHA


Leo nilienda kula mahali. Muhudumu aliyenihudumia alionekena kabisa ndio kaanza kazi ingawa ni mtu mzima kiasi. 
Tukiwa wateja wachache tu kama meza mbili au tatu bado alionekana kutaabika asijue namna ya kujigawa. 


Alipokuja kunisikiliza nilimpa order ya kinywaji kwanza kwasababu hakuna na hakika kama chakula nilichoagiza kitapatikana. Akaniahidi anakwenda kuuliza halafu atarudi. Akaondoa, aliporudi akarudi na kinywaji bila glass. 
Hakuwa ameshaulizia chakula, akasema anafata glass then ndiyo aendee kuulizia chakula. 
Alipoondoka hakurudi na baada ya muda nikaona anahudumia meza nyingine. Baadae akarudi na glasi nikamshukuru, lakini nafikiri akawa amesahau kama nilitaka chakula pia. 
Wakati ananiletea glasi vijana flani aliokuwa anawahudumia mwanzo wakaanza kumfokea. Ikabidi aende huko. Bahati akapita muhudumu mwingine nikamuita nikamuagiza chakula. Wakati nakula vurugu zikawa zimepungua nikamuita yule muhudumu wa mwanzo niongee nae zaidi. 
Akaniambia ni kweli ndio ameanza kazi na hajawahi kufanya kazi kama hii hapo awali. Nikaona huruma sana, nikamwambia kazi zote zinachangamoto zake, kuna kupuuzwa, kudharauliwa, kukejeliwa, kukataliwa, kuonekana hutoshi n.k ila fahamu yote hayo yakiwa yanatokea kuna watu hata kama ni wachache ambao watathamini kazi na huduma yako. HAO WACHACHE WATOSHE KUKUTIA MOYO NA UENDELEE KUFANYAKAZI KWA KUJIAMINI. 
Nikamaliza nikamshukuru nikaondoka. Watu hawafanani kwa hiyo tunaweza kufanikiwa kwa pamoja kama, tutavumiliana, tutaelekezana kwa upendo na kupeane moyo.

Na Elinasi Monga.Copyright 2007-2017 @KAJUNASON BLOG


Source: KajunasonRead More